Atletico Madrid yaiponda Bayern Munich UEFA

Haki miliki ya picha Getty

Michuano ya Kombe la Klabu Bingwa barani Ulaya hatua ya nusu fainali imeendelea tena jana, Atletico Madrid wakipata ushindi dhidi ya Bayern Munich katika dimba la Vicente.

Atletico walichomoza na ushindi wa bao 1-0, bao lililofungwa na Saul Niguez.

Timu hizo zitarudiana tena wiki ijayo ikiwa ni mchezo wa mwisho kuweza kumpata mshindi atakayecheza hatua ya fainali ya michuano.