Arsenal kuivaa Norwich city-EPL

Haki miliki ya picha Getty

Ligi kuu ya soka ya England inaendelea tena hapo kesho kwa michezo kadhaa.

Everton ni wenyeji wa Bournemouth, Newcastle United wanawaalika Cristal Palace,Stoke city dhidi ya Sunderland,Watford watachuana na Aston Via,West Brom wanawaalika West Ham United, na Arsenal watakuwa wenyeji wa Norwich city.

Hadi sasa ligi hiyo inaongozwa na Leicester city yenye alama 76,Tottenham alama 69,Man city alama 64 sawa na Arsena yenye alama 64.

Katika nafasi ya mwisho katika msimamo Timu za Aston via na Newcastle ndio Timu zinazoburuza mkia kufuatia kuwa na alama chache kuliko Timu zote.

Idhaa ya Kiswahili ya BBC itakutangazia mechi kati ya New castle Unite na Cristal palace.