Tigers yatwaa taji Namibia

Haki miliki ya picha Getty

Klabu kongwe ya Namibia Tigers, imemaliza ukame wa miaka 31 baada ya kutwaa ubingwa wa msimu wa 2015/2016 wa ligi kuu nchini humo.

Baada ya kulikosa mara kadhaa kombe, hatimaye klabu hiyo imetwaa taji kwa kishindo huku wakiwa wamebakiza mechi mbili na kuzima utawala wa Timu za Black Africa na African Stars, ambazo zimekuwa zikitawala soka ya Namibia kwa miaka saba iliyopita.

Licha ya kufungwa 3-2 na Citizens, lakini wamefanikiwa kutwaa ubingwa kwa kufikisha pointi 67, sita zaidi ya Black Africa inayoshika nafasi ya pili katika ligi ya timu 16.

Timu hiyo imefungwa mechi tatu tu kati ya 30 msimu huu, ikishinda 20 na sare saba.

Kwa matokeo hayo, Tigers itaiwakilisha Namibia katika Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani.