Newcastle yanusurika,Sunderland yapata sare

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Wachezaji wa Newcastle

Klabu ya Newcastle imaimarisha matumaini yake ya kusalia katika ligi kuu ya Uingereza kufuatia bao la Andros Townsend na penalti iliopanguliwa na kipa wa kilabu hiyo dhidi ya Crystal palace.

Huku Norwich ikicheza dhidi ya Arsenal na Sunderland kutoka sare na Stoke,Newcastle sasa imepanda hadi nafasi ya 17 na kuondoka katika eneo la kushushwa daraja.

Towsend aliipatia Newcastle bao la kwanza baada ya mapumziko kupitia shambulio kali.

Kipa Darlow baadaye aliokoa Newcastle alipookoa penalti ya Yohan Cabaye.