Rayon Sports wazidisha matumaini Rwanda

Rayon
Image caption Rayon Sports wana mechi moja hawajacheza

Katika ligi kuu ya soka nchini Rwanda Rayon Sports imejijengea matumaini ya kuweza kuibuka na ubingwa msimu huu kwa kucharaza hasimu wake mkubwa APR kwa magoli 4-0 uwanja wa taifa Amahoro.

Mchezaji kutoka Uganda Kasulya Davis ndiye aliyekuwa nyota wa mchezo huo kwa kunusa nyavu mara tatu.

Goli hilo jingine lilitiwa kimiani na mshambuliaji Diarra kutoka Mali.

APR, ambayo ni timu ya majeshi, bado inaongoza ligi kwa kuizidi Rayon Sports kwa alama 1 lakini Rayon Sports ina mechi ya kiporo.