Amir Khan: Sina nguvu za kumuumiza Alvarez

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Amir Khan

Bondia Amir Khan amekiri kwamba hana nguvu za kumjeruhi Saul Canelo Alvarez katika pigano lao la WBC uzani wa kati mjini Las Vegas siku ya Jumamosi.

Hatahivyo raia huyo wa Uingereza amesema kuwa kasi yake ndio itakayoshinda pigano hilo.

Amir Khan mwenye umri wa miaka 29 ataruka mizani miwili ili kukabiliana na Alvarez ,ijapokuwa mechi hiyo itapiganiwa katika uzani wa kilo 70.

''Nitampiga Canelo na huenda asisikie ngumi zangu lakini ujuzi ndio utakamshinda'',alisema Khan.

''Sitaki kushiriki katika kurushiana makonde,kusimama mbele yake na kumpa fursa ya ya kuinipiga'',ninajua anaweza kuniumiza na ngumi moja kali.

Image caption Saul Alvarez

''Kwa hivyo lazima niwe chonjo nitakaporusha ngumi zangu .Ni nidhamu na kuhakikisha kuwa ninaendelea na mpango wangu wa mechi hiyo hadi raundi ya 12''.

''Mbeleni,sikuwaheshimu mabondia ambao wamenibwaga sakafuni.Pigano hili najua naweza kujeruhiwa kwa hivyo nitakuwa chonjo na kujilinda''.

''Pigano dhidi ya Mayweather au Manny Pacquiao lingekuwa rahisi kwangu kwa sababu tuko sawa kwa urefu kwa hivyo ningekuwa na nguvu kimwili.Canelo atakuwa na nguvu lakini vitu nilivyojihami navyo ni kasi na mwendo''.