Dembele apigwa marufuku mechi sita

Mousa Dembele Haki miliki ya picha Rex Features
Image caption Dembele sasa atakosa mechi za kwanza za msimu ujao

Kiungo wa kati wa Tottenham Hotspur Mousa Dembele amepigwa marufuku mechi sita na Shirikisho la Soka la Uingereza.

Ameadhibiwa baada ya kupatikana na kosa la kumshambulia mchezaji wa Chelsea Diego Costa.

Dembele, ambaye huchezea timu ya taifa ya Ubelgiji, alionekana kumfinya macho mshambuliaji huyo wa Chelsea wakati wa mechi ambayo iliisha kwa sare ya 2-2.

Mwamuzi Mark Clattenburg hakumuadhibu mchezaji huyo wa kiama 28 wakati wa mechi hiyo.

Dembele aliamua kutopinga shtaka hilo na sasa hataweza kuchezea klabu yake, ambaye mkufunzi wake ni Mauricio Pochettino, hadi mechi ya tano msimu ujao.

Amechezea Spurs mechi 29 ligini msimu huu na kuwafungia mabao matatu.

Dembele alikuwa miongoni mwa wachezaji tisa wa Spurs waliooneshwa kadi ya manjano wakati wa mechi hiyo iliyochezewa Stamford Bridge.

Hiyo ni rekodi kwa wachezaji wengi zaidi kuadhibiwa kwenye mechi moja Ligi ya Premia.