MOJA KWA MOJA: Norwich dhidi ya Man United

Wenyeji Norwich wanaialika mabingwa wa zamani wa ligi ya Uingereza Man United katika kiputi ambapo timu zote zinahitaji pointi kwa udi na uvumb ili kusonga mbele.

Matoke ya EPLNewcastle 0-0 Aston VillaSunderland 3-2 ChelseaNorwich 0-1 Manchester United Crystal Palace 2-1 StokeWest Ham 1-4 SwanseaNa maechi inakamilika hapa huku Man United wakichukua pointi zote tatu na hivyobasi kujipatia matumaini

16.29pm:Baada ya kupotea katika kipindi cha kwanza Wayne Rooney amerudi na nguvu mpya na amekuwa na ushawishi mkubwa hapa katika safu ya mashambulizi ya Man United

16.24pm:Ilikuwa Rooney aliyewachanganya mabeki wa Norwich halafu akatoa pasi nzuri kwa Mata aliyekaribia lango na kumwacha kipa wa Norwich bila Jibu.

dakika ya 38 ya kipindi cha pili.Norwich 0-1 Man United

16.18pm:Goooooooooooal Man United wapata bao hapa kunako dakika ya 23 kupitia Juan Mata

16.07pm:Norwich wanaanza kufanya mashambulizi na Mbokani anakosa kichwa cha wazi hapa .namna gani.ilipigwa krosi safi na mbokani akabakia na goli lakini akapiga kichwa cha juu

16.06pm:Norwich inafanya mabadiliko upande wa mashambulizi na Mbokani mchezaji wa DRC anaingia.

16.01pm:Man United wanajaribu kuvizia ngome ya Norwich kwa gusa ni guse nje ya boksi lakini Walinzi wa Norwich wanajipanga na kuzuia mashambulizi

Image caption Norwich dhidi ya Man United

16.00pm:Manchester United wananza kwa moto hapa katika kipindi cha pili cha mechi.

15.45pm:Kipindi cha kwanza chakamilika

14.27pm:Safu ya ulinzi ya Norwich yakataa.Norwich inashambulia sasa lakini anaanguka mshambuliaji katika eneo la hatari la Man United

Image caption Norwich dhidi ya Man United

15.25pm:Norwich 0-0 Manchester United

15.24pm:Manchester United wapata kona nyingi lakini hakuna mazao yake. dakika ya 39

15.19pm:Norwich wanatafuta bao pale katika lango la man united dakika ya 34

Image caption Norwich dhidi ya Man United

15.17pm:Kumbuka kwamba iwapo man United watashindwa mechi ya leo matumaini yao ya kushiriki katika ligi ya vilabu bingwa yatadidimia kwa asilimia kubwa.

Hatahivyo itategemea mechi ya kesho kati ya Arsenal dhidi ya manchester City uwanjani Anfield

15.15pm:Chris smalling akosa bao la wazi hapa kufuatia kona.wachezaji wa man United wanajaribu kupitia kila pembe .

Wanajaribu kupiga mikwaju ya nje ya boksi lakini bahati haijasimama.

Image caption Rooney

15.10pm:Kona nyengine kuelekezwa Norwich.Ziko wapi huduma za Wayne Rooney haonekani akishika mpira

15.05pm:Kona kuelekezwa Norwich,Mabeki wanazuilia pale na kupiga mpira kuelekea lango la Man United.Hatari sana hawa vijana wa Norwich wanaposhambulia.

14.53pm:Norwich 0-0 manchester united

Image caption Norwich dhidi ya manchester United
14.49pm: Kumbuka Norwich inahitaji alama za kulitoka eneo la kushushwa daraja hapa huku man United ikitafuta nafasi ya kushiriki katika mechi za vilabu bingwa ulaya.
Image caption Norwich
15.47pm:Mechi inaanza huku Norwich ikianza kwa mashambulizi katika lango la manchester United
Image caption Kikosi cha Man United
14.45pm:Norwich vs Manchester United