Lennox Lewis:Amir Khan anaweza kumshinda Canelo

Image caption Aliyekuwa Bondia wa uzani mzito duniani Lennox Lewis kushoto

Bondia wa zamani kutoka nchini Uingereza Lenox Lewis amesema kuwa Amir Khan anaweza kumshangaza Saul Canelo Alvarez siku ya Jumamosi iwapo atacheza mchezo wake.

Khan mwenye umri wa miaka 29 ameruka mizani miwili ili kukabiliana na mpinzani wake kutoka Mexico katika uzani wa kati mjini Las Vegas.

Katika onyesho la upimaji uzani wawili hao walikuwa na kilogramu 70.

Image caption Canelo Alvarez kushoto na Amir Khan kulia

''Khan anaweza kushinda iwapo hatamruhusu Canelo kumfikia karibu.Khan ni bondia mzuri ,anatembea vizuri katika jukwaa na kurusha ngumu nzuri,Lakini atahitaji kudhibiti matembezi yake dhidi ya Canelo sio kukimbia bila mpango.Na pia lazima ujue kwamba sio yeye pekee ataingia ulingoni na mkufunzi wake''.