Serengeti boys yaelekea India

Timu ya vijana ya Tanzania chini ya umri wa miaka 17 Serengeti boys imeondoka jana kwenda Goa India.

Timu hiyo inakwenda kushiriki michuano maalumu ya soka ya kimataifa kwa vijana (AIFF Youth Cup 2016 U-16) yaliyoandaliwa na Shirikisho la Soka la nchini India (AIFF)

Timu hiyo imeondoka na kikosi cha wachezaji 22,ratiba ya michuano inaonyesha kwamba Tanzania itafungua dimba na Marekani.

Serengeti Boys watashuka dimbani tena Mei 17, kucheza na wenyeji India.

Kisha Mei 19 watacheza dhidi ya Korea Kusini na mchezo wa mwisho watamaliza dhidi ya Malysia Mei 21.

Fainali ya michuano hiyo itachezwa Mei 25 ambapo kabla ya mchezo wa fainali, utachezwa mchezo wa mshindi wa tatu katika uwanja huo huo Tilak Maidan, Vasco, Goa nchini India.