Jeraha lamuweka Welbeck nje kwa miezi 9

Haki miliki ya picha PA
Image caption Welbeck

Mshambuliaji wa klabu ya Arsenal na Uingereza Danny Welbeck hatocheza kwa miezi tisa baada ya kufanyiwa upasuaji kutokana na jeraha la goti.

Welbeck mwenye umri wa miaka 25 alipata jeraha la mguu wake wa kulia wakati timu yake ilipopata sare ya 2-2 dhidi ya Manchester City siku ya jumapili na hatocheza mchuno wa Euro 2016.

Klabu yake imesema kuwa ukaguzi uliofanywa umebaini kwamba aliumia vibaya na kwamba sio jeraha la hapo awali lililomfanya kukosa miezi saba ya msimu huu.