Serena, Djokovic washinda

Nyota wa mchezo wa Tenesi Serena Williams ametinga hatua ya robo fainali katika michuano ya wazi ya Italia.

Serena licha ya hali ya ugonjwa iliyosababishwa na kuonja chakula cha mbwa wake amepata ushindi wa seti mbili kwa kumshinda mpinzani wake Christina McHale kwa 7-6 na 6-1,

Nae mwingereza Johanna Konta akaputwa nje ya michuno hiyo baada ya kuchapwa na Misaki Doi wa Japan kwa seti ya kwanza alishinda kwa 4-6 kisha akapoteza kwa 7-5 na 6-2.

Kwa upande wa wanaume Andy Murray amesonga mbele baada ya kumshinda Jeremy Chardy kwa 6-0 6-4, hivyo Murray atachuana na David Goffin, aliyemshinda Tomas Berdych kwa 6-0 6-0.

Roger Federer akatupwa nje na Dominic Thiem kwa kupoteza kwa 7-6 (7-2) 6-4.Thiem atakutana na Kei Nishikori, hatua inayofuata .

Nae nyota namba moja kwa ubora Novack Djokovic alimshinda Tomaz Belluci kwa kwa seti 6-3, 6-2 huku akipoteza seti ya kwanza kwa 0-6, Djockovic atachuana na Rafael Nadal aliyemshinda Nick Kyrgios kwa 6-2 na 6-4.