Pep Guardiola: Nimeimarika zaidi

Haki miliki ya picha AP
Image caption Pep Guardiola

Kocha wa Bayern Munich Pep Guardiola anasema kuwa amekuwa kocha bora zaidi katika misimu yake mitatu katika klabu hiyo wakati ambapo anajiandaa kucheza mechi yake ya mwisho katika ligi hiyo.

Kocha huyo wa zamani wa kilabu ya Barcelona ambaye ameshinda ligi ya Bundesliga katika miake yake mitatu anajiunga na klabu ya Manchester City msimu ujao.

''Nimejifunza mengi kutoka kwa wachezaji wangu.Ninafurahia uamuzi wangu wa kuja hapa''.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Pep Guardiola

Mechi ya Jumamosi kati ya Bayern Munich na Hannover ndio mechi yake ya mwisho katika uwanja wa Allianza Arena.

Mechi yake ya mwisho itakuwa mechi ya kombe la Ujerumani kati ya timu yake na Borussia Dortmund Jumamosi ijayo huku akitarajia kushinda kombe la pili katika kipindi cha miaka mitatu.