Sevilla watwaa kombe ligi ya Europa

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Sevila wabeba kombe la Europa

Klabu ya soka ya Sevilla ya nchini Hispania imeshinda taji la Europa kwa mara ya tatu mfululizo baada ya kuichabanga klabu ya soka ya Liverpool kutoka Uingereza magoli matatu kwa moja.

Liverpool walitawala na kuongoza kipindi cha kwanza lakini Sevilla walisawazisha matokea mwanzoni kabisa mwa kipindi cha kwanza na baadaye kufunga magoli mawili ya ushindi.

Kwa ushindi huo wa Sevilla itamaanisha kuwa vilabu vya nchi ya Hispania vitatawala katika mashindano makubwa msimu huu.Fainali ya klabu bingwa barani Ulaya itachezwa Mei 28 baina ya Real Madrid na Atletico Madrid.