Chris Eubank Jr kumpa taji lake Blackwell

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Blackwell

Bondia wa uzani wa kati Chris Eubank amejitolea kumpatia ukanda wake kwa bondia mstaafu Nick Blackwell kama hatua ya ukarimu .

Blackwell mwenye umri wa miaka 25,alivuja damu katika ubongo katika pigano alilopoteza kwa Eubank mnamo mwezi Machi na kukaa bila fahamu.

Ombi hilo linajiri licha ya Blakwell kusema kuwa Eubank na babaake hawana 'utu' kuhusu vile walivyochukulia jeraha lake baada ya pigano hilo.

''Nilifupisha kazi yake'',Eubank aliiambia ITV nchini Uingereza.

''Alisema kuwa kila kitu kiko sawa na kwamba hakuna hisia zozote mbaya,lakini nilimzuia kujipatia kipato''.

Image caption Blackwell

''Nilitaka kuja ili kumuona kwa kuwa nilikuwa na kitu chake na kwamba kitu hicho ni ukanda wangu wa Uingereza''.