Varane kuikosa michuano ya Euro

Haki miliki ya picha Reax Features
Image caption Raphael Varane

Beki wa timu ya taifa ya Ufaransa Raphael Varane ameachwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo.Varane hajajumuishwa kwenye kikosi kitachoshiriki michuano ijayo ya Euro itayoanza mwezi June kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya nyama za paja.

Pia nyota huyu wa klabu ya soka ya Real Madrid ataukosa mchezo wa fainali ya kombe la klabu bingwa ulaya utapigwa Mei 28 kati ya timu yake na Atletico Madrid.

Mchezaji huyu atakua nje ya uwanja kwa muda wa wiki tatu mpaka nne na nafasi yake kwenye kikosi cha taifa imechukuliwa na beki wa Adil Rami, mwenye umri wa miaka 30 anayeichezea timu ya Sevilla ya nchini Hispania.