Yanga mabingwa wa shirikisho

Image caption Yanga ilipomenyana na Azam Fc

Klabu ya soka ya Yanga, imetwaa ubingwa wa tatu kwa msimu huu baada ya kutwaa ubingwa wa kombe la shirikisho kwa kuichapa Azam, kwa mabao 3-1.

Mchezo huu uliopigwa kwenye dimba la taifa jijini Dar es salaam, ulishudia kikosi cha Yanga, ilipata ushindi wake kupitia kwa magoli ya mshambuliaji Amisi Tambwe aliyefunga bao la kwanza katika dakika ya tisa ya kipindi cha kwanza kisha akaongeza bao la pili katika dakika ya 47 ya kipindi cha pili .

Katika dakika ya 81 winga Deus Kaseke, alihitimisha kazi kwa kufunga bao la tatu baada ya kuunganisha krosi ya Simon Msuva.Bao la kufutia machozi la Azam,liliwekwa kambani na mshambuliaji Didier Kavumbagu.

Licha ya Yanga kushinda mchezo huu wa fainali Azam ndio wataiwakilisha Tanzania katika michuano ijayo ya kombe la shirikisho huku Yanga wakiwakilisha katika michuano ya klabu bingwa Africa.