Zlatan Ibrahimovic aitwa na kilabu ya Uingereza

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Zlatan Ibrahimovic

Aliyekuwa mshambuliaji wa klabu ya PSG nchini Ufaransa Zlatan Ibrahimovic amesema kuwa alipokea ombi la kujiunga na kilabu moja ya ligi ya Uingereza lakini akakataa kuthibitisha iwapo klabu hiyo ni Manchester United au la.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 yuko huru baada ya kuondoka PSG na amehusishwa na uhamisho wa United.

Alipoulizwa iwapo ombi hilo linatoka Old Trafford ,alisema :Wacha tuone kitakachofanyika.

Image caption Mourinho na Ibrahimovic

Aliyekuwa kocha wa Chelsea Jose Mourinho anatarajiwa kutangazwa mkufunzi wa Manchester United na alifanya kazi na Ibrahimovic alipkuwa katika kilabu ya Inter Milan.