Man United na Mourinho wakubaliana

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Jose Mourinho

Makubaliano ya mkufunzi Jose Mourinho kuwa kocha wa kilabu ya Man United msimu ujao yameafikiwa baada ya mazungumzo ya siku tatu.

Majadiliano kati ya ajenti wa Mourinho Jorge Mendes na maafisa wakuu wa United yamekamilika ijapokuwa hakuna kandarasi iliotiwa saini.

Tangazo rasmi kutoka kwa klabu hiyo linatarajiwa siku ya Ijumaa.

Raia huyo wa Ureno atachukua mahala pake Louis van Gaal,ambaye alifutwa kazi siku ya Jumatatu, siku tatu baada ya United kushinda kombe la FA