Andy Murray sasa kucheza jumatano

Haki miliki ya picha AP
Image caption Andy Murray mchezaji wa Tennis

Mchezo wa nusu fainali kati ya Andy Murray na Richard Gasquet umesogezwa mpaka siku ya Jumatano kutokana na hali mbaya ya hewa. Mchezaji huyo namba moja wa Uingereza hapo awali alikiri kuwa mvua kali inayoendelea kunyesha isingeweza kumzuia kuingia dimbani lakini haikuwa hivyo. Mvua zinatarajiwa kupungua katika jiji la Paris baada ya siku mbili. Mvua hizo kubwa zimesababisha droo ya mzunguko wa nne kwa wanaume na wanawake iliyotarajiwa kufanyika siku ya jumatatu kusogezwa mpaka Jumatano.