Bekele aachwa nje ya kikosi cha Rio de Janeiro

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kenenisa Bekele

Bingwa wa zamani wa mbio ndefu duniani Haile Gebreselassie ameshtumu shirikisho la riadha nchini Ethiopia kwa kumwacha bingwa mara tatu wa mashindano ya Olimpiki Kenenisa Bekele nje ya kikosi cha taifa hilo kinachoelekea katika michezo ya Olimpiki ya Rio de Jeneiro mnamo mwezi Agosti.

Haile aliambia BBC kwamba Bekele alifaa kuorodheshwa katika kikosi cha Marathon bila pingamizi yoyote kutokana na rekodi yake nzuri.

Shrikisho la riadha nchini Ethiopia linasema kuwa Kenenisa aliwachwa kwa kuwa hakuafikia mahitaji ya kikosi hicho.

Image caption Gabresellassie

Kenenisa amekosoa uamuzi huo akisema haukuwa wa haki.

Bekele alikuwa wa tatu katika mashindano ya Lonmdon marathon mnamo mwezi Aprili,licha ya kutofanya mazoezi kamili na alishinda mbio za marathon za Great Manchester Run mwezi uliopita.