Ulaghai wa kodi: Messi atakiwa kutoa ushahidi

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Messi na babake wakiwa mahakamani

Nyota wa soka wa timu ya Argentina na Barcelona Lionnel Messi anatarajiwa kutoa ushahidi katika mahakama ya Uhispania kuhusu mashtaka ya kukwepa kulipa ushuru.

Messi na Babake Jorge ambaye anasimamia maswala yake ya fedha wanatuhumiwa kuilaghai Uhispania zaidi ya yuro milioni 4 kati ya mwaka 2007 na 2009.

Mamlaka inadai kuwa wawili hao walitumia kampuni zao zilizopo Belize na Uruguay kuficha mapato yao yanayotokana na haki za picha zao.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Messi

Mamlaka ya ushuru nchini Uhispana inataka mchezaji huyo kupigwa faini kubwa pamoja na kufungwa jela.

Wawili hao wamekana kutekeleza uhalifu huo.