Mashindano ya Olympic angalizo latolewa

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Bendera za mashindano ya Olympic

Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa imetangaza hatua mpya zitakazolenga kuondoa udanganyifu wa matumizi ya dawa za kuongeza nguvu michezoni katika michuano ya Olimpiki mjiji Rio de Janeiro.

Kamati hiyo imesema kuwa itaongeza bajeti ya vipimo hususan kwa wanariadha kutoka Urusi, Kenya na Mexico.

Nchi hizi tatu zimekuwa chini ya viwango vilivyowekwa na shirika la kupambana na dawa zilizopigwa marufuku michezoni.

Kamati hiyo pia imeahidi kuendelea na upelelezi wa sampuli za awali katika michuano ya Beijing na London.

Mpaka sasa zaidi ya wanaridaha 50 wanatuhumiwa kwa matumizi ya dawa hizo huku 22 wakitokea Urusi.Maamuzi ya iwapo wanariadha wa Urusi watashiriki michuano ya Rio mwaka huu yatatolewa baadae mwezi huu.