Wakimbizi 10 kushiriki Olimpiki Rio de Janeiro

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Misenga atashiriki katika Judo

Kamati ya kimataifa ya Olimpiki imetangaza majina ya wanariadha kumi wakimbizi watakaoshiriki katika michezo ya Olimpiki ya Rio de Jeneiro,kikiwa ni kikosi cha kwanza cha wakimbizi kushiriki Olimpiki.

Wanariadha watano wanatoka Sudan Kusini,wawili kutoka Syria,wawili wengine kutoka DRC na mmoja kutoka Ethiopia.

Baadhi yao watashiriki katika uogeleaji,wengine Judo na wengi katika michezo ya uwanjani.

Timu hiyo itakuwa nyuma ya bendera ya Olimpiki na iwapo mmoja wa wanariadha hao watashinda medali wimbo wa michezo ya Olimpiki utachezwa.

Kamati ya Olimpiki IOC imesema kuwa imeanzisha kikosi hicho kutoa ujumbe wa matumaini kwa wakimbizi duniani.