Majina sawa ya wagombea yakanganya Romania

Vasile Cepoi Haki miliki ya picha AP
Image caption Wagombea watatu wanaitwa Vasile Cepoi

Wakazi wa mji mmoja nchini Romania hawataweza kutumia majina kuwatofautisha wagombea wakati wa kumchagua meya kwani wagombea watatu wanafanana majina.

Uchaguzi wa meja katika mji huo wa Draguseni, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo utafanyika Jumapili.

Vasile Cepoi, anayewania muhula wan ne, ni miongoni mwa wagombea. Lakini kuna wagombea wengine wawili wenye jina sawa na lake, wanaitwa Vasile Cepoi.

Cepoi ni jina maarufu sana la kiukoo eneo hilo na jina Vasile ni maarufu pia kwa wanaume nchini Romania.

Wapiga kura watahitajika kutumia picha na nembo za wagombea pamoja na kuangalia kwa makini majina ya vyama ndipo waweze kufanya uamuzi sahihi wakat iwa kupiga kura.

Baadhi ya vyombo vya habari vimesema huenda ni njama ya vyama vingine kuhakikisha wagombea wao wanachaguliwa.

Mji wa Draguseni una wakazi 1,200.