Andy Murray ahitaji mapumziko zaidi

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Andy Murray

Katika Tenisi Andy Murray amesema angependa kuyapa kipaumbele mapumziko katika kuelekea Wimbledon baada ya kupokea kipigo kutoka kwa Novak Djokovic katika French Open.

Hili ni taji la kwanza la French Open kwa Mserbia Djokovic na anakuwa mtu wa kwanza wa kizazi hiki kuwa na rekodi ya kuwa na Grand Slams nne kwa wakati mmoja. Mara ya mwishi rekodi ya namna hiyo alikuwa nayo Rod Laver mwaka 1969