World Cup groups

GROUP B: ARGENTINA

Manager: Diego Maradona

Key player: Lionel Messi

Best: Winners (1978, 1986) odd

World ranking:

Timu ya Argentina chini ya meneja wake Diego Maradona ambaye ameonekana kuwa katika wakati mgumu baada ya kukabiliana na shinikizo kadhaa, ilipitia changamoto kubwa kabla ya kufuzu kucheza kombe la dunia

Hatahivyo fursa adimu katika kipindi hicho kigumu ilipatikana huko Uruguay, kwa goli la Mario Bolatti lililopatikana katika dakika za mwisho ambalo na kuwa la ushindi 1-0 wa kujipatia tiketi ya kwenda Afrika Kusini.

Katika historia, Argentina imewahi kushindwa kufuzu kucheza kombe la dunia mara moja tu, 1970. Lakini ushindi wao wakati huu umeipatia nafasi ya nne na ya mwisho katika kundi lao la Amerika ya Kusini.

Wakati wakionekana kuwa goigoi kuliko wakati mwingine wowote katika kumbukumbu za kombe la Dunia, huwezi kwa uhakika kufutilia mbali nafasi iliyowapa sifa kwa kupambana na vipaji vya wachezaji wa Barcelona 2009, kama vile Ballon d'Or winner Lionel Messi, Atletico Madrid's Sergio Aguero na Angel di Maria wa Benfica.

Sera za meneja kuhusu uteuzi wa wachezaji pia ni suala linalozua udadisi na ni vigumu kuzitetea sera zake. Wakati huohuo, hapana shaka, wana uwezo wa kuwa washindani, lakini bado ni vigumu kutabiri mambo yatakavyowaendea huko Afrika Kusini. Vyovyote vile itakavyokuwa huko uwanjani, kwa upande wa Maradona itakuwa ni safari yenye mvuto.

NIGERIA

Manager: Shaibu Amodu

Key player: Yakubu Aiyegbeni

Best: Round two (1994, 1998)

World ranking:

Nigeria ilifuzu kucheza kombe la dunia kwa kishindo cha aina yake baada ya kuishinda Kenya 3-2 huko Nairobi. Super Eagles ilipaswa kushinda ili kuizuia Tunisia isifuzu. Walisawazisha goli baada ya Kenya kuongoza 1-0 na baadaye ikaongoza bao lingine, na matokeo kuwa 2-1, lakini katika dakika ya 79 wakaruhusu goli la kusawazisha, ni Obafemi Martins aliyefunga goli la ushindi baadaye na kumaliza mchezo.

Super Eagles walijawa na bahati nyingi katika harakati za kufuzu kwenye kundi lao, kwa kutoka sale katika mechi zao tatu, ikiwa ni pamoja na ile waliocheza na Tunisia, na hawakufanya kosa kuonesha furaha yao hatimaye. Hata hivyo ubora wa timu hiyo ulijidhihirisha mwishoni. Kwa hali yoyote ile, Nigeria inajivunia wachezaji mahiri kama mlinzi wa timu ya Everton Joseph Yobo, Kiungo wa Chelsea Jon Obi Mikel na washambuliaji duo Martins na Yakubu ambao kwa viwango vyao, watakuwa ni hatari kwa timu nyingi, lakini wachezaji wote kwa pamoja watapaswa kujinoa iwapo watahitaji kupata mafanikio kama ya kipindi cha nyuma.

SOUTH KOREA

Manager: Huh Jung-Moo

Key player: Park Ji-Sung

Best: Fourth (2002)

World ranking:

South Korea ilipata nafasi ya saba yenye mafanikio katika kufuzu kucheza fainali za kombe la dunia, kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya United Arab Emirates huko Dubai. Wakiwa wameshinda mechi nne na sale nne, wakiwa na magoli manne na kufuzu ni ishara ya timu hiyo kuwa na maandalizi ya kutosha wakiwa na dhamira na uwezo wa kumaliza kazi.

Chini ya uongozi wa Guus Hiddink, South Korea kwa umaarufu mkubwa ilijitengenezea njia kucheza nusu fainali za kombe la dunia 2002 wakiwa nyumbani, baada ya kuzishinda timu za Ureno, Itlia na Spain. Kuna mashaka ya kuwapo uwezekano wa kurudia historia hiyo Afrika Kusini na kufanya vyema zaidi katika hatua za makundi. Kiuongo wa Manchester United Park Ji-Sung ndiye kapteni na mcheza nyota wa timu hiyo, ingawa kiwango chake kizuri hakiwezi kuziba udhaifu wa nafasi zingine.

GREECE

Manager: Otto Rehhagel

Key player: Giorgos Karagounis

Best: Round one (1994)

World ranking:

Machampioni wa kombe la ulaya 2004 Ugriki (Greece), ilifuzu kucheza kombe la dunia tangu 1994. Shukrani kwa kocha veterani Otto Rehhagel, ambaye ndiye aliyeweka mipango ya ushindi huko Ureno. Wakimaliza wakiwa katika nafasi ya pili kwenye Kundi la Pili, nyuma ya Switzerland, ambayo iliishinda mara mbili, walikutana na Ukraine katika mchuano mkali na kushinda 1-0 huko Donetsk baada ya sale ya 0-0, huko Athens, kwa Dimitrios Salpigidis akiwa juu.

Rehhagel ni mtaalam wa kukuza vipaji vya wachezaji anavyokuwa navyo. Aliongeza zaidi hadhi ya ushujaa wake huko Ugriki kwa kutoa maelekezo kushika nafasi ya pili kucheza fainali za Kombe la Dunia, na kunauwezekano wa kufanya vyema zaidi kupitia udhaifu wa 1994. kepteni na kiungo wa Liverpool Giorgos Karagounis ndiye atakayekuwa nguzo ya timu huko Afrika Kusini, wakati mlinzi wa Liverpool Sotirios Kyrgiakos akicheza nafasi yenyekuhitaji mtindo wa mshikamano.

Wala siyo kitu kilichopo juu ya uwezo wake kutikisa miamba ya timu kwa mara nyingine, lakini pia siyo kwamba hakuna uwezokano kwa timu hii kuomea raundi ya kwanza kwa mara nyingine.