Viwanja vya Afrika Kusini

Uwanja wa Royal Bafokeng Sports Palace ni moja ya viwanja vitavyotumika kwa ajili ya Kombe la Dunia 2010. Uwanja huo umepewa jina la watu wa jamii ya Bafokeng wanaoishi katika eneo hilo.

Mwaka 1999 jamii ya Ki-Bafokeng walishinda mapambano ya kisheria yaliowapa nguvu za kupata mrabaha wa asilimia 20 kutokana na madini ya platinum ambayo yanachimbwa katika eneo lao la jadi. Na kwa hivyo sasa wana hisa katika uchimbaji wa madini hayo muhimu kiviwanda na kisayansi.

Uwanja huo utakuwa na uwezo wa kuingiza watu 42,000. Timu ya Bafana Bafana ilitumia uwanja huo mwaka 2001 kwa ajili ya michuano ya kufuzu ya Kombe la Dunia na kushinda 2-1. Uwanja huo umekaribisha mechi kadhaa za Ligi Kuu ingawa mji wenyewe wa Rustenburg hauna timu ya Ligi Kuu.

Uwanja huo uko masafa ya dakika 25 tu kutoka Sun City na dakika 30 hivi kutoka Pilansberg. Na ulipo uwanja huo ni kilomita 12 kutoka kati kati ya jiji la Rusterberg.

Uwanja wa Ellis Park uko katikakati ya jiji la Johannesburg na umekaribisha shughuli kadhaa za michezo na mechi kadhaa kubwa ikiwamo fainali ya Kombe la FIFA la Mabara 2009 katika ya Brazil na Afrika Kusini.

Kiwanja kimefanyiwa marekebisho makubwa kabla ya michuano hiyo ya Kombe la Mabara na kwa sasa inaweza kuingiza watu 62,000 ikiwa ni nyongeza ya asilimia 9 ya uwezo wake wa zamani wa viti 57,000.

Ellis Park awali kabisa ulijengwa mwaka 1928 kutumika kuwa kiwanja cha mchezo wa raga. Ukavunjwa na kujengwa upya mwaka 1982, na wakati huo pia kufanywa maalum kwa mchezo huo huo wa raga.

Uwanja huo ukapewa jina la JD Ellis, diwani wa mmoja katika jiji la Johanesburg ambaye ndie aliyetoa kibali cha kuruhusu ardhi kutumika kwa ujenzi wa uwanja huo ambao umeenea katika ukubwa wa eka 13.

Uwanja huo utabaki katika nafasi maalum kwenye nyoyo za wapenzi wa michezo wa Afrika Kusini kwa sababu ndio uwanja ambao Afrika Kusini waliilaza New Zealand katika fainali ya Kombe la Dunia la mchezo wa raga hapo 1995 ikiwa ni muda mdogo tu baada ya milango ya Afrika Kusini kufunguliwa kushiriki michezo ya kimataifa baada ya kufungiwa kwa miongo kadhaa kutokana na ubaguzi wa rangi

Michuano hiyo lilikuwa ni tukio lilowaleta watu wa Afrika Kusini pamoja na picha ya Nelson Mandela akinyanyua Kombe hilo la dunia ilionyeshwa dunia nzima.

Katika kiwanja hicho ni ubazi wa kaskazini ndio uliofanyiwa kazi zaidi na kuchangia kwa kiasi kikubwa katika kuongeza idadi ya mashabiki wanaoweza kuingia na kufikia 62,000. Ikiwa na vifaa vya kisasa kama vile huduma kwa waandishi wa habari, vyombo vya hali ya juu vya wachezaji, eneo mwanana la wageni maarufu, fursa ya urahisi wa kuingia na kutoka kwa watu wenye ulemavu, vipaza vinavyotoa taarifa kwa wepesi kwa watazamaji, kila mtu atastarehe kuingia katika uwanja huo.

Ellis Park ni uwanja wa timu maarufu kuliko zote Afrika Kusini yaani Orlando Pirates FC.

Uwanja wa Nelson Mandela Bay ukiwa katika fukwe za Ziwa North End ni wa mwnazo katika mji huo au eneo la karibu ya hapo. Kiwanja hiki ni kipya kabisa ambacho kimejengwa maalum kwa ajili ya Kombe la Dunia 2010, na kimekamilika mapema kwa mwaka mzima kabla ya michuano hiyo mikubwa duniani, na hilo likiwa ni la mafanikio makubwa kwa mji huo

Uwanja huo wa Nelson Mandela Bay utakuwa mwenyeji kwa mechi moja ya robo fainali na moja ya kutafuta mshindi wa tatu. Uwanja huo una umbo la paa la kuvutia na umesarifiwa kukabiliana na mandhari ya kuvutia ya ziwa la North End.

Kabla ya kujengwa uwanja huo ambao utaweza kutumika kwa shughuli mbali mbali, mechi zote za soka za kimataifa zilikuwa zikichezwa katika uwanja waraga wa JImbo la Mashariki unaoitwa Uwanja wa EPRU.

Kiwanja cha kuchezea kitakuwa cha majina ya asili wakati maeneo ya pembeni ya uwanja yatakuwa ni ya nyasi bandia. Moja ya mechi za majaribio katika kiwanja hicho ilikuwa ni mpambano wa mahasimu wa jadi wa Soweto katika kila kinachoitwa Soweto Derby na timu hizo zikiwa ni Orlando Pirates na Kaizer Chiefs- ambapo mchezo kama huwa haubakishi kiti kitupu uwanjani.

Huu ni mmoja ya viwanja vilivyosanifiwa vyema huko Afrika Kusini na ni uwanja mpya kabisa ukijengwa katika moja ya eneo la kifahari katika mji wa Cape Town.

Uwanja wa Green Point utakuwa mwenyeji wa mechi moja wapo ya hatua ya nusu fainali.

Uwanja huo utaoweza kutumika kwa shughuli mbali mbali umeshapangwa kutumika kwa shughuli kubwa na matamasha. Watazamaji watakuwa masafa madogo tu kutoka maeneo ya pwani na milima ya Cape Town ikitoa mandhari nzuri kwa upande wa nyuma.

Chagua la eneo hilo limesadifu na kuwa karibu sana na kitovu cha usafiri katika mji huo. Kiwanja hicho kimejengwa kwa kumega kwa kiasi fulani eneo ambalo lilikuwa likitumika kwa mchezo wa gofu.

Uwanja huo uliojengwa kwa teknolojia ya kuta za nje zenye kupunguza kelele uan uwezo wa kuchukua watizamaji 70,000 na tayari umekamilika kwa wakati uliopangwa

Eneo la Green Point Common, ambalo uwanja huo umejengwa, zamani ilikuwa ni kubwa kuliko lilivyobaki hivi sasa, na lilijumuisha sehemu kubwa ya ardhi baina ya Signal Hilo na kunyoosha kuelekea eneo la kati kati ya jiji kwenda Sea Point.

Cape Town ina kiwanja chengine kinachoitwa Newlands, lakini hiki hutumika zaidi kwa shughuli na mechi za raga. Baada ya Kombe la Dunia inatarajiwa kuwa uwanja huu mpya utatumiwa na vilabu vikubwa vya mji huo kama vile Ajax Cape Town na pia timu ya Santos.

Jina la uwanja huo limetokana na mmoja wa wanaharakati wa ukombozi dhidi ya utawala wakibaguzi. Uwanja wa Peter Mokaba ina historia ya kipekee nchini Afrika Kusini. Peter Mokaba alizaliwa na kukua mjini Polokwane na alijulikana kutokana na ari yake ya kupigania haki na uongozi wake wenye kuhamasiha watu.

Uwanja huo umejengwa kwa kutumia zege na kujengwa kwa kufuata taswira ya mbuyu, huku paa la uwanja huo likishikiliwa na nguzo za chuma katika kila upande wa uwanja. Uwanja huo umejengwa karibu kabisa na uwanja wa zamani wa Peter Mokaba, huko Polokwane katika jimbo la Limpopo. Uwanja huu mpya upo karibu kilomita 5 tano kutoka katikati ya jiji.

Msghambuliaji wa kimataifa wa Ivory Coast, Didier Drigba alicheza mchezo wake wa kwanza wa kimataifa kwenye uwanja wa zamani wa Peter Mokaba, dhidi ya Afrika Kusini, katika michuano ya kombe la Mataifa ya Afrika, ambapo Afrika Kusini ilishinda kwa mabao 2-1.

Uwanja wa Loftus Versfeld, upo mjini Tshwane/Pretoria ni uwanja wa zamani zaidi nchini Afrika Kusini. Uwanja huo umetumika kwa shughuli mbalimbali za kimichezo tangu mwaka 1903. Sehemu ya kwanza kabisa ya uwanja huo ambayo ilikuwa ina uwezo wa kuchukua watazamaji 2,000, ilijengwa na Halmashauri ya Jiji la Pretoria mwaka 1923.

Tangu mwaka 1948, uwanja huo umefanyiwa ukarabati mara kadhaa. Aidha umetuumika kwa ajili ya michezo ya rugby na soka, na ni uwanja wa nyumbani kwa timu ya rugby ya Blue Bulls. Loftus Versfeld upo katikati ya mji wa Tshwane/Pretoria. Uwanja huo umetumika kwa ajili ya michezo kadhaa mikubwa, ikiwa ni pamoja na Kombe la Dunia la mchezo wa rugby mwaka 1995 na mwaka 1995 katika Kombe la Mataifa ya Afrika. Pia uwanja huo unatumika kama uwanja wa nyumbani kwa timu za Mamelodi Sundowns na SuperSport United.

Timu ya taifa ya Afrika Kusini, Bafana Bafana, ilipata ushindi wake wa kwanza dhidi ya timu ya taifa ya Sweden bao 1-0 mwaka 1999.