Rooney haondoki Trafford

Sir Alex Ferguson na Wayne Rooney
Image caption Rooney amebadilisha nia na kuamua kuendelea kuichezea Man U

Baada ya kuzozana, meneja wa klabu ya soka ya Manchester United, Sir Alex Ferguson, hatimaye amefanya mapatano na mshambulizi Wayne Rooney, na mchezaji huyo kukubali kuendelea kusalia uwanja wa Old Trafford, hadi mwezi Juni, mwaka 2015.

Leo amesema amesema amezungumza na meneja na wamiliki wa klabu, na wamemshawishi kwamba yeye klabu bora zaidi kinachomfaa ni Man U.

Siku chache zilizopita Rooney, alikuwa ametangaza kwamba hana nia ya kuendelea kuichezea Man U.

Siku ya Jumatano, mshambulizi huyo mwenye umri wa miaka 24, alikuwa ameelezea nia yake ya kuondoka, kutokana na wamiliki wa klabu kukosa kumhakikishia juu ya mipango ya kuimarisha kikosi cha timu.

Meneja wa Man U, Sir Alex Ferguson, ameelezea kufurahishwa na uamuzi huo wa Wayne Rooney wa kutia saini mkataba wa miaka mitano.

Kwa zaidi kuhusu ligi ya Premier, kuwa nasi Jumapili, katika Ulimwengu wa Soka, wakati tutakapokutangazia mechi kali kati ya Manchester City na Arsenal, mechi mbili za awali zikiwa ni Stoke kucheza na Manchester United, na Liverpool ikiikaribisha Blackburn.