Mashabiki saba wafariki uwanjani Nairobi

Mashabiki saba wamekufa katika uwanja wa soka wa Nyayo, mjini Nairobi, kufuatia mkanyagano katika uwanja wa Nyayo.

Image caption Afisa wa usalama na mashabiki katika uwanja wa Nyayo

Habari za awali zilikinukuu kituo cha matangazo cha Jambo FM.

Hayo yalitokea katika mechi ya ligi kuu ya Kenya, kati ya timu za Gor Mahia na AFC Leopards.

Kulingana na kituo hicho ambacho kwa kawaida hutangaza moja kwa moja mechi za soka, watu hao saba walikufa baada ya mashabiki kujaribu kuingia uwanjani kwa kutumia mabavu, ili kutizama mechi hiyo ya vilabu hivyo vikongwe, ambavyo ni kati ya vilabu maarufu zaidi vya soka nchini Kenya.

Kituo cha matangazo cha Jambo FM kilielezea kwamba licha ya vifo hivyo vya mashabiki hao saba kutokea, mwamuzi hakusitisha mechi hiyo.

Mechi hiyo pia ilichezwa katika mazingira ya mvua kubwa.