Odemwingie awa mwingi kwa Newcastle

Mabao mawili kutoka kwa Peter Odemwingie yaliiwezesha West Brom kupata ushindi dhidi ya Newcastle katika uwanja wao wa The Hawthorns.

Image caption Mabao yake mawili kati ya matatu yaliyofungwa yaliweza kuiletea ushindi mkubwa WBA

Bao la kwanza lilikuwa la Sunderland, wakati kiungo cha kati, Somen Tchoyi, alipata bao baada ya nusu saa.

Baadaye Odemwingie alipata nafasi nzuri baada ya kosa la Danny Guthrie kuutema mpira, na aliweza kumpita Tim Krul na kupiga mkwaju wa chini kwa chini.

Mchezaji huyo kutoka Nigeria aliweza kutia wavuni bao lake la pili katika mechi hiyo ya Jumapili, kabla ya Peter mwenzake, Peter Lovenkrands, kupata bao la kujituliza la Newcastle.

West Brom walionyesha kuwa na mchezo bora zaidi, na wakishambulia kwa jitihada kubwa.