Beckham kujiunga na Tottenham au la?

Mchezaji hodari, Beckham
Image caption Mchezaji hodari, Beckham

Huenda Beckham hatajiunga na Tottenham ilivoytarajiwa hapo awali.

Tangazo limewabumbuwaza wengi kwani Redknapp, Ijumaa hii, alisema kuwa maafikiano ya kumsajili Beckham yalishakamilishwa kwa asilimia 90.

Mchezaji huyo, aliye na umri wa miaka 35 sasa, angekuwa katika mchuano hii leo, uwanja wa White Hart Lane.

Meneja wa Spurs amekatishwa tamaa kwa kukosa kumsajili Beckham, kwani taathira atakayoleta Beckham kwa vijana wa klabu hiyo itasaidia kuleta msukumo ili kuwapa nafasi katika ligi ya klabu bingwa.

Image caption Meneja wa Spurs, Redknapp

Redknapp amesema 'Tungependa kuwa naye kwa mda mrefu huku tukiheshimu majukumu aliyonayo kwa LA Galaxy.'

'LA Glaxay walimhitaji Beckham kuanzia mapema Februari na hili likaleta pigo katika kufikia mwafaka wa kumsajili kwa wiki tatu.'

'David ni mchezaji bora na ataleta taathira kubwa hapa na nimeshawishika kuwa sote tutanufaishwa na ujasiri wake na atatupa shime ya ushindani.'

'Nadhani kila mtu hapa atafurahishwa na Beckham kuwa miongoni mwetu.'

Beckham aliwahi kufanya mazoezi na Spurs, mahasimu wa Arsenal, mjini London,na huenda ataanza kazi wiki hii katika uwanja wa mazoezi Essex na anangojea kwa hamu kujiunga nao.

Image caption Wachezaji wa timu ya Spurs

Beckham alisema 'Ni muhimu kufanya mazoezi na kuwa katika hali nzuri kiafya wakati wa mwisho wa msimu huu.

Ninawashukuru Tottenham na Harry Redknapp kwa kunipa fursa hii kufanya mazoezi na timu hii katika kipindi cha mwezi mmoja ujao.

Ninawashukuru LA Galaxy pia kwa kunipa fursa hii ya kufanya mazoezi na Spurs na nina hamu sana ya kufanya kazi nao hivi karibuni.'

Ingelikuwa Beckham amejiunga na Spurs, angelikuwa ni kati ya wachezaji wa timu hiyo na wangelichuana na timu ya Manchester United, timu yake ya zamani, Jumapli ijayo katika uwanja wa White Hart Lane.