Pele aipigia debe Tottenham Spurs

Mchezaji soka maarufu wa zamani kutoka Brazil, Pele, ameingilia ubishi kuhusu umiliki wa uwanja wa Olimpiki wa mjini London, baada ya mashindano ya mwaka 2012.

Image caption Spurs na Hammers wanautaka uwanja wa Olimpiki

Pele anaipigia debe klabu ya Tottenham.

Vilabu vya Tottenham na West Ham siku ya Ijumaa viliwasilisha barua zao za mwisho rasmi kutaka kuumiliki uwanja huo, katika eneo la mashariki mjini London.

Katika barua aliyoiandika, Pele anaunga mkono mipango ya Tottenham ya kutaka kuondoa sehemu ya uwanja ya riadha, na kuukarabati kabisa kwa kuufanya uwanja wa soka.

Kampuni inayohusika na usimamizi wa uwanja, Olympic Park Legacy Company (OPLC), tayari ilikuwa imepokea mapendekezo ya awali kutoka kwa vilabu hivyo viwili.

Ombi la Spurs pia limepata nguvu kwa kuungwa mkono na mchezaji mwingine wa zamani, Jimmy Greaves, ambaye aliweza kuifungia Tottenham magoli 220 katika jumla ya mechi 321 games for Spurs.