Bolton 2 Everton 0

Daniel Sturridge
Image caption Sturridge ameiwezesha Bolton kushikilia nafasi ya nane katika ligi ya Premier

Daniel Sturridge aliweza kuandikisha bao lake la tatu katika mechi tatu, na kuiwezesha timu yake ya Bolton kupata ushindi dhidi ya Everton, katika mchezo wa uwanja wa nyumbani wa Reebok.

Wenyeji walipata bao la kuongoza wakati Gary Cahill alipoukimbia msukumano wa wachezaji, na kuuelekeza kwa kichwa mkwaju wa wapinzani wa free-kick kutoka kwa Stuart Holden, hadi katika lango lake mwenyewe.

Tim Cahill angeliweza kusawazisha, lakini alishindwa kuupokea vyema mpira kutoka kwa mwenzake Leighton Baines.

Lakini Sturridge, mwenye umri wa miaka 21, tangu kujiunga na Bolton mwezi uliopita wa Januari, aliweza kuthibitisha umahiri wake wa kushambulia kutokana na Bolton kupata free-kick.

Mchezaji huyo wa mkopo kutoka Chelsea, ambaye aliingia uwanjani baada ya muda, alithibitisha kwamba akipata nafasi ya kuanza mechi mapema anaweza kucheza mchezo wa kuvutia.

Sturridge hakupata nafasi nzuri kuichezea Chelsea katika uwanja wa Stamford Bridge.

Ushindi wa Bolton umemfurahisha sana meneja Owen Coyle na wachezaji wake, kwani timu yake sasa imo katika nafasi ya nane ya ligi kuu ya Premier.