Libya kukosa uhondo

BBC ina inafahamu kwamba Libya sasa haitawezak kuandaa michuano ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 20.

Image caption Huenda Afrika Kusini au Ghana ikatakikana kuokoa jahazi

Mashindano hayo yalitazamiwa kuanza tarehe 18 mwezi wa Machi mwaka huu.

Wimbi la kutaka mabadiliko ya kijamii na kisiasa nchini Libya limelilazimu shirikisho la soka barani Afrika, CAF, kufikiria kuyahamisha mashindano hayo.

Taarifa ambazo imezipata BBC zinagusia kwamba huenda mashindano sasa yakafanyika aidha Afrika Kusini, au Ghana.

Tarehe mpya ya kufanyika mashindano hayo, na uamuzi wa nchi itakayoandaa mashindano hayo, itatangazwa mara tu CAF itakapokata kauli.

Libya imekuwa katika mzozo katika kipindi cha wiki moja iliyopita, na mgawanyiko miongoni mwa raia, na waandamanaji wakimtaka Kanali Gadaffi kuondoka madarakani.