West Ham yakataa kuwa ya mwisho

Scott Parker
Image caption Scott Parker

Scott Parker aliweza kuipa moyo timu yake ya West Ham, ambayo iliongeza juhudi na kuweza kuifanya timu hiyo ya mashariki mwa jiji la London kuacha kushikilia nafasi ya mwisho mwa ligi kuu ya Premier.

Parker aliweza kufunga bao la kwanza la mechi katika dakika ya 22, na kuiwezesha West Ham kutangulia.

Demba Ba naye aliweza kuuwelekeza mpira katika lango la Liverpool, na kuiwezesha timu ya Hammers kuendelea kuongoza kwa magoli 2-0.

Liverpool walijikakamua, na katika dakika ya 84, Glen Johnson alifanikiwa kuifungia Liverpool bao la kujituliza, na licha ya wageni wakiwa na matumaini, mkwaju wa Carlton Cole ulikamilisha mechi hiyo kwa ushindi wa West Ham.

Liverpool's late rally resulted in Glen Johnson tapping in after 84 minutes but Carlton Cole drove in a shot to secure a valuable win for the Hammers.