Fabregas kucheza dhidi ya Barcelona

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, amesema ana imani Cesc Fabregas ataweza kucheza mechi ya Jumanne ya klabu bingwa, dhidi ya Barcelona.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Wenger anasema ana imani atacheza dhidi ya Barca

Hili ni pambano la timu 16 zilizosalia katika mashindano hayo.

Wenger atawakosa wachezaji kadha katika pambano hilo la uwanja wa Nou Camp, wakati ambapo Arsenal itajaribu kuutetea ushindi wake ilipocheza nyumbani, na kuongoza magoli 2-1.

Lakini kuhusiana nahodha wake aliyejeruhiwa na ambaye anatazamiwa kupimwa zaidi, Wenger alisema: "Kwa asilimia 90 ninaamini atacheza".

"Kurudi kwake ni muhimu katika kushambulia na vile vile ulinzi".

Fabregas hakuwepo uwanjani katika mechi ya ligi kuu ya Premier ya England dhidi ya Sunderland siku ya Jumamosi, na timu ilitoka pasipo kufungana mabao katika mechi hiyo, na wakitazamiwa kupata ushindi na kuwasumbua zaidi Manchester United.