Fabregas anukuliwa vibaya

Arsene Wenger
Image caption Amekasirishwa na jarida la Uhispania

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, amesema kamwe hatabadilisha msimamo wake, kwamba jarida la Uhispania "lilipindapinda" maneno aliyoyasema Cesc Fabregas baada ya kufanya mahojiano naye.

Katika mahojiano hayo, Fabregas ilielekea anamhujumu meneja Wenger, na maelezo ya taarifa ya Don Balon ilielezea kwamba Fabregas aliyatamka hayo kwa "uaminifu mkubwa".

Lakini Wenger alijibu kwa kusema: "Kile wanachokisema hakituvutii kabisa, hawakuheshimu makubaliano tuliyoyafanya".

"Kamwe hawatapata tena mahojiano nasi, kabisa."

Katika mahojiano hayo, inadaiwa Fabregas alielezea kwamba ikiwa Wenger angelikuwa ni meneja wa klabu kidogo nchini Uhispania, ikifikiriwa kwamba timu ya Arsenal ya "Gunners" haijawahi kupata ushindi, tangu kufanikiwa kupata Kombe la FA mwaka 2005.

"Ni wazi kwamba ukija Uhispania na useme Unai, (kocha wa Valencia), Emery, (Pep wa Barcelona) Guardiola au Mourinho (Jose wa Real Madrid), kwamba hawatashinda kombe lolote katika kipindi cha miaka mitatu, basi ni wazi hawataweza kuendelea (na kazi zao)", alinukuliwa Fabregas, kiungo cha kati wa timu ya taifa ya Uhispania, na mwenye umri wa miaka 23.

Matamshi ya Wenger ya haraka ilikuwa ni kumlaumu mwandishi, akisema "aliyapindapinda maneno ya Fabregas na tumekerwa mno na hayo".