Man Utd 1 - 0 Everton

Javier Hernandez Haki miliki ya picha AFP
Image caption Aiwezesha Man U kuukaribia ubingwa wa Premier

Javier Hernandez aliweza kuifungia Manchester United bao katika dakika za mwishomwisho za mechi ya kwanza Jumamosi, na kuiwezesha kuongeza tofauti ya pointi tisa kati yao na wapinzani katika ligi kuu ya Premier, baada ya kuishinda Everton. Sylvain Distin aliiwezesha Man U kupata mpira, na Hernandez kuiadhibu Everton, ikiwa zimesalia dakika saba kabla ya mechi kumalizika, baada ya kuutia golini mpira wa kichwa kutoka kwa Antonio Valencia.

Awali, mara mbili Hernandez aliweza kuitisha Everton, lakini mlinda lango Tim Howard aliweza kuokoa mikwaju hiyo.

Lakini Everton huenda wakamlaumu mwamuzi, kwa kudai aliwanyima nafasi ya kupiga penalti alipoangushwa Victor Anichebe.

Ingawa Howard alifanya juhudi kubwa katika kuokoa mikwaju ya Man U, hatimaye juhudu zao zilifua dafu.

Wachezaji wa Sir Alex Ferguson sasa wanahitaji kujikusanyia pointi saba kutoka mechi nne zilizosalia, kunyakua ubingwa wa ligi kuu ya England kwa mara ya 19.