Mourinho anachafua sifa ya Real Madrid

Aliyekuwa Rais wa klabu ya Real Madrid Ramon Calderon amesema kuwa sifa ya klabu hiyo kwa sasa imechafuliwa na tabia ya kocha wake Jose Mourinho wakati wa pambano la nusu fainali ya Ulaya dhidi ya Barcelona.

Haki miliki ya picha 1
Image caption kocha alaumiwa kwa kuchafua sifa ya klabu

Real imetupwa nje ya mashindano hayo na mahasimu wake wakuu Barcelona ingawa michuano ya duru mbili iligubikwa na matukio ya ghasia za mashabiki, wachezaji na wakuu wa vilabu.

Kinara Mourinho alionyesha kadi nyekundu katika duru ya kwanza kwa kuhoji adhabu ya kadi nyekundu akikabiliwa na tatizo la matamshi yake.

Rais wa zamani wa Real Madrid, Calderon ameiambia BBC kuwa matamshi yake ni sumu na yanaiathiri Real Madrid.

Mechi ya kwanza ilitawaliwa na fujo zilizotokea wakati wa mapumziko ya kipindi cha kwanza wachezaji walipokua njiani kuelekea vyumba ambapo goalkeeper wa akiba Pinto wa Real Madrid kuonyeshwa kadi nyekundu.

Baadaye klabu hiyo ilikiona baada ya kubaki na wachezaji kumi baada ya Pepe kuonyeshwa kadi nyekundu kwa kumchezea vibaya Dani Alves.

Hatimaye Mourinho naye akaonyeshwa kadi nyekundu kwa matamshi yake kwa msaidizi wa mwamuzi alipomsifu baada ya tukio hilo. Aliendelea na kilio chake kusema kuwa ni bayana kuwa dhidi ya Barcelona, huwezi kupata fursa yoyote ya ushindi. Sijui kama ni kwa sababu ya kuwa wanavaa nembo ya shirika la Unicef, au ni wazuri sana lakini wana nguvu kiasi hicho.

Labda ni urafiki wa Rais wa chama cha mpira cha Uhispania(Angel Maria kwenye shirika la soka barani Ulaya ambako ni makamu wa Rais. Mourinho alinungunika akisema ushawishi wa wakuu kama hao huenda unaifanya Barcelona kuwa hivyo ilivyo.

Matamshi yake na vurugu kati ya vilabu hivyo ilipelekea Uefa kuvichukulia hatua.

Calderon amemlaumu Mourinho kwa kile alichozua kwa matamshi yake kuhusu Uefa na mwamuzi wa mechi na kusema hayakubaliki.