Man U kumpokea Phil Jones

Mlinzi wa Blackburn Rovers, Phil Jones, anatazamiwa kujiunga na Manchester United, kufuatia makubaliano ya pauni milioni 17.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Anatazamiwa kuichezea Manchester United

Mchezaji huyo wa timu ya England ya vijana chini ya umri wa miaka 21 yumo katika kuchunguzwa afya yake na mabingwa wa ligi kuu ya Premier, baada ya awali kukataa kujiunga na Arsenal wala Liverpool.

Jones alicheza kwa mara ya kwanza katika ligi kuu ya Premier mwezi Machi, lakini alithibitisha anaumudu mchezo wa kandanda katika kipindi cha msimu mmoja.

Mchezaji huyo wa miaka 19 alitazamiwa kusafiri Jumatano na kikosi cha England cha vijana chini ya umri wa miaka 21 katika michuano ya Ulaya nchini Denmark.