Mishahara soka ya England inapanda

Kiwango cha gharama za vilabu vya Ligi kuu ya Premier nchini England juu ya mishahara kimekithiri na kufikia rekodi ya asili mia 68 katika msimu wa mwaka 2009-10, kwa mujibu wa ripoti inayochunguza matumizi ya fedha katika mchezo wa soka na kampuni ya Deloitte.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Sir Alex Ferguson

Wakati Manchester United ilitumia asili mia 46 ya mapato yake kulipa mishahara, watani wao Manchester City walitumia asili mia 107 ya mapato.

Licha ya kiwango hicho cha kutisha bado Chelsea ilikithiri kama kawaida yao tangu msimu wa mwaka 2002-03, wakimwaga pauni za Uingereza milioni 174.

Image caption Chelsea yaongoza malipo makubwa

Hali hii inaleta wasiwasi, jambo ambalo linafaa kufanyiwa uchunguzi na sheria za Uefa za kusawazisha viwango vya matumizi ya fedha kwa vilabu vya soka.

Ripoti hii inatokea wakati ripoti ya Deloitte inaonyesha kuwa mapato kutokana na Ligi ya Premier yameongzeka kwa asili mia 2% na kuzidi pauni bilioni 2 za Uingereza katika msimu wa 2009-10.

'Mishahara ya wastani' Bw.Jones amesema kuwa kulikuepo na ishara za tabia nzuri katika ulipaji mishahara miongoni mwa vilabu vilivyo katika sehemu ya kati na chini katika vilabu vya Ligi kuu, ingawa vile vilivyo kileleni vilifanikiwa kimapato na hilo likasaidia kusawazisha viwango vya mishahara.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Vilabu vidogo vinatii sheria

Tatizo linabaki kati ya vilabu ambavyo vipo tu haviwanii nafasi ya kushiriki mashindano ya Uefa au havimo hatarini kushuka daraja.

Pamoja na yote hayo bila shaka Manchester City na Chelsea itabidi kutizama tena mishahara yao kuambatana na sheria ya malipo yanayostahili.