Savic Beki wa pili baada ya Clichy

Klabu ya Manchester city imekamilisha usajili wa beki mwingine Stefan Savic kutoka klabu ya Partizan Belgrade.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 ni beki wa pili kusajiliwa na Man.city baada ya Gael Clichy kutoka Arsenal.

Ikumbukwe kuwa Savic aliwahi kufanya majaribio ya siku kumi kwenye klabu ya Arsenal mwaka jana na badala ya kutia saini na klabu hiyo amesahihisha mkataba wa miaka minne na klabu ya kaskazini mwa England.

Kijana huyo alishiriki mchuano wa Timu yake ya Taifa ya Montenegro katika mchuano dhidi ya England kwenye uwanja wa Wembley mnamo mwezi Oktoba mwaka 2010 katika mechi ya kufuzu kushiriki fainali za Euro 2012.

Vilevile aliwahi kushiriki michuano iliyoshirikisha vilabu vya Ligi ya Premier akiwa na klabu yake ya Partizan ilipochuana na Arsenal katika Ligi ya mabingwa barani Ulaya mwezi Disemba.