Odemwingie aisaidia Brom

Peter Odemwingie Haki miliki ya picha AP
Image caption Ameanza vyema msimu kwa kuiwezesha West Brom kupata ushindi baada ya kuugua

Peter Odemwingie, baada ya kurudi uwanjani kufuatia jeraha, na kuanza kwa kishindo msimu huu kwa kuisaidia West Bromwich Albion kuepuka kuteremshwa daraja, kwa kuifunga Norwich bao 1-0 katika uwanja wa ugenini.

Norwich, ambao kufikia sasa hawajafanikiwa kuishinda timu yoyote katika ligi ya Premier, walianza mechi kwa wasiwasi, na kutoa nafasi kwa mshambulizi huyo kutoka Nigeria kupata bao, baada ya kupokea mpira kutoka kwa Nicky Shorey, katika dakika ya tatu ya mchezo.

Graham Dorrans alikuwa nusra apata bao la kusawazisha, kabla ya mlinda lango wa Norwich, Declan Rudd, kuweza kuoka mkwaju wa penalti kutoka kwa Odemwingie katika nusu ya pili ya mchezo.

Peter Odemwingie alisema: "Ilikuwa ni mchezo mgumu - ilikuwa wazi kwa kila mtu kwamba ilibidi tujitahidi. Lakini ilikuwa muhimu tupate ushindi ugenini baada ya kushindwa katika mechi tatu."

"Nilifurahi sana kufunga. Nilikuwa sijiamini, lakini kwa kufunga chini ya dakika tano za mwanzo, niliwaza kutuliza mawazo, na hilo liliweza kunisaidia katika mechi nzima", alieleza Odemwingie.

Katika mechi ya pili iliyochezwa siku ya Jumapili, mashabiki karibu 25,000 katika uwanja wa Craven Cottage waliweza kutizama mechi kati ya Fulham na Blackburn, iliyokwisha kwa sare ya 1-1.

Bao la kwanza katika mechi hiyo lililikuwa la Blackburn, na lilifungwa na Ruben Rochina katika dakika ya 32.

Fulham walisawazisha katika dakika ya 38, kupitia Bobby Zamora.