Swansea yashinda mchuano wake

Klabu iliyopanda daraja msimu huu ya Norwich ikitumia ujanja wa msisitizo wa kuendelea kucheza mfumo wao imeichapa Bolton na kuiongezea majonzi klabu hio.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Matokeo mengine ya mechi za jumamosi

Juhudi za Canaries(jina la utani la Swansea) katika kipindi cha kwanza zilifanikiwa kwa bao la Anthony Pilkinton mnamo dakika ya 38 likifuatiwa na la kichwa la Bradley Johnson dakika sita baadaye.

Bolton ikapungukiwa mchezaji mmoja baada ya Ivan Klasnic kumtuta kichwa Marc Tierney. Mnamo dakika ya 64 kipindi cha pili machungu ya Bolton yalizidi kwa adhabu ya mkwaju wa penalty.

Kwenye uwanja wa Wolves, mashabiki walitarajia muendelezo wa ushindi lakini mfululizo wa magoli kupitia Joey Barton na Alejandro Faurlin yakifuatiwa na bao la dakika za majeruhi la DJ Campbell yaliwaacha mashabiki wa Wolves wakishangaa jinsi gani klabu iliyopanda daraja msimu huu ilivyoweza kuwacharaza matatu bila kuwa na ujanja wa kujibu.

Kwenye uwanja wa Villa Park klabu ya Aston Villa ilianza vyema kwa bao la mapema ingawa Newcastle ilirudisha na mechi kumalizika 1-1.