QPR yafurahia sare dhidi ya Aston Villa

Adel Taarabt
Image caption Adel Taarabt kutoka Morocco ni kati ya wachezaji walioitisha mno Aston Villa siku ya Jumapili

Queens Park Rangers walifanikiwa kupata pointi moja wakati wa muda wa majeruhi walipoweza kupata bao la kusawazisha, kupitia Richard Dunne kufunga katika lango lake mwenyewe, katika mechi ambayo wageni Aston Villa tayari walikuwa wakiongoza kwa bao moja.

Wageni waliweza kuvuma katika kipindi cha kwanza, huku Adel Taarabt akiwa nusra kupata bao, na mkwaju wa free-kick wa Bannan ukishindwa kuzaa matunda.

Bannan hata hivyo alipata nafasi nyingine, wakati huu kupitia mkwaju wa penalti, katika dakika ya 58, baada ya Armand Traore kumchezea vibaya Gabriel Agbonlahor.

Licha ya Villa kuondoka kwa sare, hata hivyo watajituliza kwa kuwa angalau rekodi yao ya kutoshindwa tangu msimu ulipoanza wameweza kuidumisha.

Dakika za mwanzo na za mwisho katika mechi hiyo, ilikuwa wazi kwamba Villa walikuwa wamelemewa na kuishiwa na mbinu muwafaka.

Meneja wa QPR Neil Warnock amewashukuru sana wachezaji wake kwa kuondoka na sare, bao la Dunne la Villa kujifunga wenyewe likiwa la kwanza katika uwanja wao wa nyumbani wa Loftus.