Chelsea yatoka sare na Velencia.

Chelsea ilipoteza alama mbili muhimu pale mchezaji wake wa akiba Salomon Kalou alipowapa zawadi ya penalti timu ya Valencia kwa kuunawa mpira kukiwa kumesalia dakika tano mechi kumalizika.

Haki miliki ya picha net
Image caption Wachezaji wa Chelsea wapambana na Velencia

Kipindi cha kwanza kilikosa msisimko ambapo matukio muhimu katika kipindi hicho yalionekana wakati Fernando Torres na Ramires waliponyimwa magoli na mlinda lango wa Velencia Diego Alves aliyekuwa imara kabisa.

Baadae Frank Lampard alipachika bao kutokana na pasi safi ya Florent Malouda.

Lakini kutokana na kosa la Kalou aliyechukuwa mahali pa Lampard, Velencia walisawazisha bao hilo kutokana na mkwaju wa adhabu uliofungwa na Roberto Soldado.

Nayo Arsenal ilipata ushindi mwembamba dhidi ya Olympiakos kutokana na mabao yaliofungwa na wachezaji wao wapya ,and Andre Santos.

Hii imemfanya mchezaji Oxlade-Chamberlain mwenye umri wa miaka 18, kuwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi wa timu kutoka uingereza kufunga bao katika mshindano ya ligi ya mabingwa bara ulaya.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Alex Oxlade-Chamberlain

Lakini kama sio juhudi za mchezaji Mikel Arteta ambae aliokoa mpira kuingia kabla hauja vuka mstari, pengine Arsenal wangelitoka sare katika mechi hiyo waliochezea uwanja wa nyumbani.

Nao mabingwa watetezi wa kombe hilo ,FC Barcelona ya Uhispania waliwabebesha timu ya BATE Borisov kapu la mabao 5-0.

Barcelona walipata ushindi huu bila kutoa jasho jingi.

Mchezaji bora wa dunia kwa miaka miwili mfululizo Lionel Messi alifunga mabao mawili katika mechi hiyo.

mabingwa mara saba wa kombe hilo AC Milan ya Italy ilichapa timu ya Viktoria Plzen kutoka Czech 2-0 .

Katika mechi iliyochezwa katika uwanja wa San Siro, Zlatan Ibrahimovic aliifungia AC Milan bao la kwanza kupitia mkwaju wa penalti. Hii ilikuwa ni katika dakika ya 53.Na dakika 13 baadae Antonio Cassano aliipatai Milan bao la pili.

Na huko ufaransa mabingwa wazamani wa kombe hilo , Olympique Marseille wamewafunga wageni wao Borussia Dortmund ya ujerumani 3-0 .

Mwamba wa Ghana Andre Ayew aliifungia Marseille mabao mawili.