Maofisa wa Caribbean kuhojiwa

Upelelezi katika mojapo ya kashfa za rushwa katika mchezo wa mpira wa miguu katika Fifa umefikia kilele.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Uchunguzi wafanywa kuhusu rushwa

Katika kipindi cha siku chache zijazo maofisa 15 kutoka kanda ya Carribean watahojiwa juu ya kuhusika kwao katika ile kashfa ya kupokea pesa ili kumpigia kura ikihusiana na aliyekua makamu wa Rais wa FIFA Mohammad Bin Hammam.

Hili ni tukio jipya katika kashfa ambayo imelikumba shirikisho linalotawala mchezo wa mpira duniani,FIFA.

Halimashauri inayosimamia maadili itasikiliza ushahidi kuhusu mkutano uliofanyika ndani ya hoteli moja huko Trinidad mapema mwaka huu.

Tayari mgombea wa kiti cha Rais wa FIFA kwenye uchaguzi uliopita Mohammad Bin Hamman ameisha fungiwa maisha kutoshiriki masuala ya kandanda kufuatia madai kua alijaribu kuwahonga maofisa wa Caribean wampigie kura.

Jack Warner aliyekuwa kinara wa mchezo huo katika kanda hio alijiuzulu wakati uchunguzi ukiendelea. Wakuu hao wawili daima wamekanusha madai ya kuhusika na rushwa.

Upelelezi wa sasa utahusiana na maofisa 15 kutoka chama cha mpira cha Caribbean. Afisa wa 16, ambaye ni Rais wa chama cha mpira cha Guyana Colin Klass alisifungiwa kwa kipindi cha miezi 26.

Uwamuzi juu ya wenzake hautarajiwi hadi Ijumaa. Upelelezi ulianza punde baada ya mwanachama wa kamati kuu ya FIFA Chuck Blazer kutoa ushahidi wa hati ikidai kua hadi dola 40,000 zilikabidhiwa kwenye mkutano huo.

Wiki iliyopita Bw.Blazer alitangaza kua ataachia nafasi yake kama Katibu mkuu wa CONCACAF, shirika linalosimamia soka Amerika ya Kaskazini na kati pamoja na visiwa vya Caribbean.