BBC Swahili

Mwanzo > Habari

Marekani yaipa Kenya ndege za kisasa

Facebook Twitter Google+
21 Julai 2012 13:32
Ndege isiyobeba rubani, drone

Taarifa kutoka Marekani zinaeleza kuwa Wizara ya Ulinzi ya Marekani itaipatia Kenya ndege nane ndogo zisizohitaji rubani, ikiwa ni sehemu ya msaada wa kijeshi kwa nchi za Afrika Mashariki, ili kuzisaidia kupambana na wapiganaji wa Kiislamu wa Somalia, al-Shabaab.

Gazeti la Wall Street Journal la Marekani limearifu kuwa Kenya itapata ndege hizo ambazo hazitakuwa na silaha, lakini zinaweza kugundua maeneo yanayofaa kulengwa na ndege au majeshi ya ardhini.

Gazeti hilo limesema ndege zisizokuwa na rubani ni sehemu ya msaada wa Marekani, pamoja na malori, zana za mawasiliano, na silaha kwa Burundi, Djibouti na Uganda.

Alamisha hii

Email Facebook Google+ Twitter