BBC Swahili

Mwanzo > Habari

Makombora toka Gaza yawaua Waisraeli

Facebook Twitter Google+
15 Novemba 2012 09:04
Majeruhi

Israel imesema kwamba Waisraeli watatu wameuwawa na kombora lililofyatuliwa kutoka Ukanda wa Gaza.

Inasema kombora hilo liliangukia jengo moja la ghorofa la makaazi mjini Kiryat Malachi, kusini mwa Israel.

Awali, inasemekana Wapelestina watatu waliuwawa katika shambulizi la ndege za jeshi la Israel dhidi ya Gaza.

Mwandishi wa BBC aliyeko Gaza anasema kuwa aliona moshi wa makombora yanayorushwa.

Mashambulizi haya yametokea baada ya Israel kumuua kiongozi mmoja wa kijeshi wa Hamas, Ahmed Jabari, pamoja na watu wengine 10 Jumatano.

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lakutana

Nalo Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limefanya mkutano wa dharura mjini New York ili kujadili mapigano hayo.

Rais wa baraza hilo, Hardeep Singh Puri wa India, alisema kwamba ni sharti mapigano hayo yakomeshwe mara moja.

Nchi za Kiarabu zilitaka baraza hilo liishtumu Israel, lakini Marekani ikasema kuwa Israel ilikuwa na haki ya kujihami dhidi ya makombora yanayorushwa na Wapelestina.

Alamisha hii

Email Facebook Google+ Twitter